Baada
ya Chama cha Wananchi (CUF) kudai kuwa uchaguzi wa marudio uliofanyika
Januari 22, 2017 ulikiuka sheria na taratibu za uchaguzi katika baadhi
ya vituo hasa vya jimbo la Dimani, na kwamba ndio sababu ya mgombea wake
Abdulrazak Khatib Ramadhan kushindwa katika uchaguzi huo.
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na kujibu tuhuma hizo za CUF huku
ikiilaumu kwa kushiriki kuuvuruga uchaguzi wa awali wa mwaka 2015.
Wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu wa
Uenezi na Itikadi CCM, Humphrey Polepole ameishauri CUF kutafuta chanzo
cha kushindwa kwake, kwani CCM haijashiriki kwa namna yoyote ile kupora
ushindi huo.
“Matokeo
ya Dimani yamedhihirisha CUF ilikua tatizo tangu uchaguzi uliopita,
2015 CCM ilipata kura 4400, CUF 2300, 2017 CCM imepata kura 4860 sawa na
78% CUF wamepata 1200 anguko la zaidi ya 50%,” amesema na kuongeza.
“CUF
wanamtafuta wa kumuwekea lawama, sisi tunasema kushindwa kwao na kura
zao kupungua lazima kuna mchawi ndani yao wenyewe hasa Zanzibar,
wamtafute huyo mchawi sisi tumewapa ushauri ili wajiweke sawa.”
Aidha,
Polepole ameeleza siri mbili za ushindi wa kishindo wa kata 19 kati ya
20 katika uchaguzi mdogo wa marudio nchi nzima, ambapo amesema kuwa
utendaji wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli pamoja
utekelezaji wa ahadi alizoahidi katika kipindi cha kampeni za uchaguzi
Mkuu wa 2015 ndio sababu ya wananchi kuchagua wagombea wa CCM kwa
kishindo.
“Rushwa,
Ufisadi, ni adui wakubwa wa serikali ya awamu ya tano, pia inatekeleza
ahadi zake zinazogusa wananchi moja kwa moja ikiwemo elimu bure kuanzia
Darasa la kwanza hadi kidato cha nne,uboreshwaji wa huduma za kijamii,
utilewaji mikopo kwa kina mama na vijana, ujenzi wa viwanda ambapo hutoa
fursa za ajira kwa wananchi wanyonge,” amesema.
Ameongeza kua “Hizo ni siri mbili kubwa zilizotufanya tushinde kata 19 na jimbo la Dimani kwa kishindo.”
“Baadhi
ya wanasiasa wanatutisha kwamba 2020 tutakutana tutaachia madaraka,
kama wanatutabiria giza, kwetu CCM tuna mwanga mkubwa unaotupa hamasa ya
kufanya kazi zaidi ili kuwaletea watanzania mabadiliko ya haraka,” amesema.
Amesema
mwelekeo wa CCM kwa sasa ni ujenzi wa chama hicho ikiwa pamoja na
kufanya uchaguzi wa viongozi ili kupata viongozi bora, wazalendo,
wanaochukia rushwa na ufisadi, ubadhirifu pamoja na watakao kuwa tayari
kusikiliza wananchi na kuwatumikia.
Polepole ,asante kwa kuyaweka sawa yanayovurungwa na Watimba Kwiri.
ReplyDeleteNi Kweli Kabisa Kwamba ... CUF Wamtafute Mchawi...Aliyeiba Kura Zao ,
mchawi wao yupo ndani ya chama chao.
Upinzani Wameisha Wamejichokesha Kwa Kupanga Uwongo .Uwongo Wao Unawatafuna.
Wananchi Hawawakubali Wanawakimbia.
Ushahidi Tosha Ni Kuona CCM Kupata viti 19 kati ya Ishirini . Upinzani Wapo Kapaa!!