Marekani
imekubali kuiuzia serikali ya Kenya ndege za kivita na vifaa vingine
vya kijeshi, kwa kima cha Dola Milioni 418 sawa na Shilingi za Kenya
Bilioni 43.5.
Tayari bunge la Congress limepitisha kufanyika kwa manunuzi hayo na kutoa leseni ya kuidhinisha hilo.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Kenya itapokea ndege hizo aina za AT-802L na AT-504 na vifaa vingine vya kivita.
Marekani
inasema ni muhimu sana kwa Kenya kupata vifaa hivyo kwa sababu ni
mshirika muhimu na wa karibu sana katika vita dhidi ya kupambana na
ugaidi hasa kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia.
Kenya
inatarajiwa kutumia silaha hizi kuendelea kupambana na kundi la Al
Shabab nchini Somalia ambalo limeendelea kutishia kuishambulia nchi hiyo
kwa kujiunga na wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM mwaka 2011.
Wiki
iliyopita, rais mpya wa Marekani Donald Trump alihoji umuhimu wa nchi
yake kuendelea kuunga mkono vita dhidi ya Al Shabab nchini Somalia,
baada ya kutofanikiwa kwa miaka 10 sasa.
Credit: RFI
Credit: RFI
0 comments :
Post a Comment