Hatariii..!!,Mlango wa Ndege ya Bombardier Q400 Wazua Kizaa zaa Angani,Abiria Wapata Hofu Kubwa..!!!



Abiria waliokuwa wakisafiri kwa ndege aina ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Mwanza kuelekea Dar es salaam, walipata hofu baada ya ndege yao kuruka na muda mfupi baadaye kulazimika kutua tena katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza

Tukio hilo lilitokea jana saa 2.20 asubuhi uwanjani hapo, baada ya ndege hiyo kuruka kisha ikatua ndani ya dakika 20

Wakati ndege hiyo ikitua, Rubani aliwataarifu abiria kuwa wanalazimika kurejea uwanjani hapo kutokana na dharura iliyojitokeza

Wakizungumza kwa sharti la kutotaja majina yao , baadhi ya watumishi wa uwanja huo walisema walishangazwa na ndege hiyo kurejea muda mfupi baada ya kuruka, hali ambayo hutokea pindi ndege inapokuwa na hitilafu ya kiufundi

"Unajua ndege nyingi huanguka wakati wa kuruka na kutua, ndiyo maana jambo hili lilitisha abiria hata wafanyakazi.

"Lakini hakukuwa hitilafu kubwa ya hatari kwani baada ya kurejea na kukaguliwa, ilionekana mlango wa mizigo ya ndege hiyo ulifungwa vibaya, hivyo kuwasha taa ya tahadhari na Rubani kuamua kutua kwa dharura"alisema mmoja wa watumishi hao

Akielezea tukio hilo, mmoja wa abiria waliokuwa uwanjani hapo ajitarajia kusafiri na ndege nyingine, alisema wakati ndege hiyo inatua kwa dharura, wafanyakazi wa uwanja huo walionekana kuchanganyikiwa

"Wafanyakazi walikuwa 'bize' mpaka tukashtuka, tulipouliza tukaambiwa ndege imeruka na kurudi kwa sababu imepata matatizo angani"alisema mfanyakazi huyo

"Ilipotua abiria wote waliteremka na wataalamu na mafundi wengine wakaanza kuikagua na mwishowe wakagundua mlango wa chumba cha mizigo ulikuwa haukufungwa vizuri

"Kwa hiyo, tatizo hilo waliteremsha na baadaye ndege iliondoka tena"alisema abiria huyo

Wakati hao wakisema hayo, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Easter Madale, alikiri kuwapo kwa tukio hilo ingawa alisema hakujua sababu zake

"Tukio hilo lipo, lakini siwezi kulizungumzia kwa sababu linawahusu watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege

"Kwa hivyo nakuomba uwatafute hao kwasababu ndio wanaojua, ingawa linaonekana halikuwa tatizo kubwa kwani baada ya kutua, ilikaa muda mfupi na kuondoka tena", alisema
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment