NA BASHIR YAKUB -
Sheria inaruhusu kutumia
ardhi ya mtu
kukopea. Kwa maana mtu
ataomba hati yako au
nyaraka yako yoyote
ile ya umiliki
halafu ataitumia kukopea. Inaitwa Rehani ya mtu wa
tatu( third party mortgage). Kifungu
cha 113 ( 2 ) cha Sheria
ya Ardhi Na, 4 ya 1999
kimeeleza kitu hiki. Hata hivyo
yapo mambo tunayotakiwa
kujua katika mchakato
huu wote.
Ili mambo yaende
vizuri kutatakiwa kuwapo mikataba
ya aina tatu
kama tutakavyoona hapa
chini.
1.MKATABA WA MKOPO.
Mkataba wa mkopo
( Loan agreement) ni
mkataba kati ya mwomba
mkopo na na
taasisi ya fedha
inayotakiwa kutoa mkopo.
Mkataba huu utakuwa
na masharti ya
mkopo kuhusu urejeshaji, muda wa
kurejesha, viwango vya riba,
adhabu za kupitisha
muda wa rejesho, muda
ambao mkopo utadumu, nini
kitafanyika iwapo mkopaji
atashindwa kurejesha, haki na
wajibu wa mkopaji
pamoja na mkopwaji.
Ifahamike kuwa
masharti ya mkopo
hayafanani. Yanatofautiana kutoka
taasisi hadi taasisi na pia yanatofautishwa na
kiwango cha mkopo
pamoja na mazingira
yote yanayouzunguka huo mchakato. Huu
ni mkataba wa
kwanza.
2. MKATABA
WA REHANI.
Huu ni mkataba
wa pili. Mkataba wa
rehani ( mortgage deed ) utakuwa ni
kati ya taasisi
ya fedha na
mtu anayeweka rehani. Kwahiyo kama
wewe unamdhamini mtu
kwa kumpa nyumba
au shamba lako
ili akakopee basi
unatakiwa kusaini mkataba
huu.
Yule ambaye jina lake
linaonekana kwenye nyaraka ya
umiliki ndiye anayetakiwa
kusaini mkataba huu.
3. MKATABA KATI
YA ANAYEDHAMINI NA
ANAYEDHAMINIWA.
Aidha usimkabidhi mtu
hati yako akakopee
bila kuwa na
makubaliano ya kisheria na
huyo mtu. Ni
hatari sana kufanya
hivi na unaweza
kupoteza na wengi
wamekwishapoteza.
Wengi wanachojali ni
mtu achukue hela benki na
wewe akupe asilimia
zako mlizokubaliana basi
muishie hapo. Ukifanya
hivi utakuwa umekosea
sana.
Wengine huaminiana tu kwa
urafiki
au undugu na kufanya
mchakato huu bila
makubaliano maalum. Hii
si sawa na
ina madhara makubwa.
Hakikisha unamsainisha
mkataba huu na hakikisha
mkataba unakuwa na vipengele muhimu na vya
kisheria vya kukulinda
wewe na mali yako.
Moja ya kipengele
muhimu ni kueleza wazi
ikiwa atashindwa kulipa
deni huko alikokopa
ni kitu gani
kitakulinda ili mali
yako isiuzwe au
hata ikiuzwa wewe
utapata nini kutoka
kwake kufidia hiyo hasara.
4. MADHARA.
Madhara makubwa unayoweza
kupata ni pale
atakaposhindwa kulipa mkopo.
Hapa bila huruma nyumba/shamba lako
litauzwa na hautakuwa
na chochote cha
kukulinda kama mdhamini.
Wengi imewatokea hii na
aidha wamekubali mali
zao ziuzwe au
wamelazimika kumlipia mtu deni ili
kuokoa mali zao.
Pia mara nyingi
watu wanaokopea mali
za watu wana
tabia ya kukimbia/kupotea au kuwa
wajeuri pale wanaposhindwa au
kuyumba katika marejesho.
Na wanakimbia wakiwa huru
kabisa wakijua kinachofuata
ni kuuza mali
ambayo kimsingi anajua sio
ya kwake na
hivyo hana la kupoteza.
Wewe usiingie katika
majaribu haya weka mpangilio mzuri wa
kisheria ikiwa utaamua
kumdhamini mtu.
5. UWEZO WA
KUZUIA MALI YAKO
ISIUZWE.
Ikiwa ulimdhamini mtu na
ameshindwa kulipa na
sasa wakopeshaji wanataka kuuza mali
unaweza kwenda mahakamani
kuzuia uuzaji. Lakini utawezaje na
hali uliusaini mkataba
wa rehani( mortgage deed).
Niseme tu utaweza
iwapo tu una
sababu za msingi
na za kisheria
na sehemu ya
kusimamia( Locus stand).
Aidha suala la
msingi kuliko yote
ni kujihadhari sana na
mpango huu wa
kudhamini kwa kutumia
mali yako kukopea. Yawezekana nawe
unataraji kutengeneza faida
kupitia hilo, ni
jambo zuri ila
hakikisha unaweka misingi
mizuri ya kukulinda wewe na mali
yako.
0 comments :
Post a Comment