Mzambia, Donald Ngoma, hivi sasa yupo
nchini kwao Zimbabwe alipokwenda baada ya kupata matatizo ya kifamilia
kufuatia msiba wa kaka yake.
Hata hivyo, nyota huyo aliondoka nchini akiwa ni majeruhi ambapo alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti aliyoyapata huko visiwani Zanzibar ambako timu hiyo ilikuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi jambo ambalo liliufanya uongozi wa Yanga umtafutie daktari maalum wa kumtibu ili aweze kupona mapema na kurejea uwanjani na hivi karibuni ulikuwa ikisubiria ripoti yake ili kujua maendeleo yake.
Lakini mpaka nyota huyo anaondoka nchini ripoti hiyo ilikuwa bado haijafika mikononi mwa Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu, ili aweze kujua maendeleo yake kama amepona au la.
Kutokana na hali hiyo uongozi wa Yanga umeingiwa hofu kubwa na unahofia kuwa unaweza kumkosa mchezaji huyo katika mechi zake zote za Ligi Kuu Bara zilizobakia lakini pia zile za Kombe la FA pamoja na za kimataifa.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimedai juzi Jumamosi uongozi wa klabu hiyo umelazimika kuwasiliana na Ngoma na kumtaka arejee nchini haraka iwezekanavyo baada ya kumalizika kwa muda aliopewa ili aweze kuendelea matibabu.
“Lakini yeye amewaambia viongozi kuwa anaendelea vizuri na wasiwe na hofu lakini pia huko alipo anaendelea na matibabu kama kawaida,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo Bavu alisema: “Ni kweli kabisa hofu ipo lakini hali yake kwa sasa ni nzuri na nimewasiliana naye jana (juzi) na nimemwambia kuwa huko alipo aendelee na matibabu ili atakaporejea awe vizuri lakini suala la kupigiwa simu na uongozi hilo mimi silijui,” alisema Bavu.
0 comments :
Post a Comment