Mkuu wa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu,
Joseph Chilongani amemweka rumande Diwani wa Bukundi, Joseph Masibuka
(Chadema) kwa tuhuma za kubomoa nyumba 20 za wananchi kwa madai ya
kujengwa katika eneo lake.
Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Jonathan Shanna alisema jana kuwa wanachunguza madai hayo kubaini kama kuna kosa ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Shanna aliwapongeza wananchi kutojichukulia sheria mkononi wakati wa ubomoaji wa nyumba hizo wilayani hapa.
Kubomolewa kwa nyumba hizo na kampuni ya udalali, kumesababisha zaidi ya kaya 100 kukosa makazi.
Hata hivyo, Chilangoni aliwataka wananchi kurejea kwenye makazi yao na kwamba gharama za ujenzi zitafanywa na diwani huyo.
Baadhi ya wakazi hao walisema nyumba za nyasi na magodoro yalichomwa moto wakati wa ubomoaji.
0 comments :
Post a Comment