Katibu wa Chadema Jimbo la
Sengerema, Deusdeth Mwigala juzi, alipata kipigo kutoka kwa vijana wa
CCM kilichosababisha apoteze fahamu baada ya kutuhumiwa kutaka kuvuruga
mkutano wa hadhara.
Kiongozi huyo wa Chadema alikuwa akipita karibu na
eneo ambalo CCM walikuwa wakiendelea na mkutano wa kampeni ya uchaguzi
mdogo wa udiwani wa Kata ya Kahumulo, akiwa na vipaza sauti alivyotumia
kutangaza mkutano wa chama chake, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni
kuvuruga usikivu.
Hata hivyo, katibu huyo alikana kuvuruga mkutano wa chama hicho akidai alikuwa umbali wa zaidi ya mita 200 kutoka eneo ambalo CCM ilikuwa ikiendesha mkutano.
Hata hivyo, katibu huyo alikana kuvuruga mkutano wa chama hicho akidai alikuwa umbali wa zaidi ya mita 200 kutoka eneo ambalo CCM ilikuwa ikiendesha mkutano.
“Wakati naendelea na kazi ya
kutangaza mkutano wa Chadema nikiwa nimeongozana na makada wengine wanne
na dereva, ghafla tulivamiwa na watu wa CCM na wakaanza kutushambulia,”
alisema Mwigala akizungumzia tukio hilo lililotokea Kijiji cha Lubanda.
Alisema wenzake
pamoja na dereva walifanikiwa kukimbia, lakini yeye alinaswa na
wafuasi hao walioendelea kumshambulia kwa kipigo.
Hata hivyo, mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo, James Kisinza alimtupia lawama katibu huyo wa
Chadema kwa kitendo cha kupita karibu na eneo la mkutano wa CCM
akitangaza mkutano wa chama chake kwa kutumia vipaza sauti na hivyo
kuvuruga usikivu.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani
Sengerema, Hassan Moshi alisema wafuasi wao walichukizwa na kitendo
hicho na kuamua kumuadhibu kiongozi huyo kwa madai kuwa alikuwa
anavuruga mkutano wao kwa makusudi.
“Viongozi tulilazimika kuingilia
kati kumwokoa asiendelee kuadhibiwa na vijana wenye hasira, lakini
ukweli ni kwamba mwenzetu alifanya kosa kwa kuingilia mkutano wa chama
kingine kinyume cha sheria,” alisema Moshi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Mwanza, Ahmed Msangi alisema ofisi yake haijapokea taarifa hizo na
kuahidi kuzitolea ufafanuzi baada ya kuzipokea kutoka Sengerema.
0 comments :
Post a Comment