Mtunza
bustani Maganga Masele, amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi
ya Rais John Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu
utendaji wao wakuliongoza taifa.
Wakili
wa Serikali Lucy Mallya amesema kuwa Desemba 22, mwaka jana Masele
akiwa Leaders Club Kinondoni jijini Dar es salaam, alitoa lugha ya
matusi dhidi ya Rais Magufuli na Samia, maneno ambayo yangeweza kuleta
uvunjifu wa amani.
Hata
hivyo baada ya kusomewa mashtaka hayo, Masele alikana kuhusika na
tuhuma hizo, ambapo Mallya alidai kuwa upelelezi haujakamilika pia
hakuna pingamizi la dhamana kwa kuwa kisheria kosa hilo linadhaminika.
Kwa
upande wake Hakimu Mwijage amesema kuwa ili mshitakiwa awe nje kwa
dhamana ni lazima awe na mdhamini mwenye barua yenye utambulisho
atakayesaini bondi ya sh 500,000.
Masele amekamilisha masharti na kuachiwa kwa dhamana,na kesi yake itatajwa Januari 24
0 comments :
Post a Comment