Timu ya Liverpool imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa Anfield baada ya kukubali kichapo cha aibu cha magoli 3-2 dhidi ya Swansea City mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu
kwa pande zote mbili baada ya kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana
kutokana kusomana kimbinu huku Liverpool wakitaka kupunguza pengo dhidi
ya vinara Chelsea huku Swansea wakitafuta njia ya kukwepa kushuka
daraja.
Kipindi cha pili kilianza kwa wenyeji kuliandama lango la wageni na katika dakika ya 48 Mshambuliaji wa Hispania Fernando Llorente’s aliifungia Swansea na dakika ya 52 Llorente’s tena alifunga bao la pili na kuwaacha Liverpool hawana la kufanya.
Magoli mawili ya kiungo mshambuliaji Roberto Firmino ya dakika ya 55 na 69 hayakuweza kuisaidia Liverpool kukwepa kipigo kwani dakika ya 74 Mshambuliaji wa Swansea Gylfi Sigurdsson’s
alipigilia msumari wa tatu na kuweza kuondoka na pointi tatu muhimu
hadi Mpira unamalizika Swansea wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli
3-2.
Kwa matokeo hayo Swansea City
wamepanda hadi nafasi ya 17 wakiwa na pointi 18 wakati Liverpool
wamebaki kwenye nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya pointi 45 huku Chelsea
akiwa kinara kwa alama 52.
Team | P | GD | Pts | |
---|---|---|---|---|
1 | Chelsea | 21 | 30 | 52 |
2 | Tottenham Hotspur | 21 | 29 | 45 |
3 | Liverpool | 22 | 24 | 45 |
4 | Arsenal | 21 | 26 | 44 |
5 | Manchester City | 21 | 15 | 42 |
6 | Manchester United | 22 | 12 | 41 |
7 | Everton | 22 | 9 | 34 |
8 | West Bromwich Albion | 22 | 0 | 30 |
9 | Stoke City | 22 | -6 | 28 |
10 | West Ham United | 22 | -8 | 28 |
11 | Bournemouth | 22 | -7 | 26 |
12 | Burnley | 21 | -8 | 26 |
13 | Southampton | 21 | -7 | 24 |
14 | Watford | 22 | -13 | 24 |
15 | Leicester City | 21 | -10 | 21 |
16 | Middlesbrough | 22 | -6 | 20 |
17 | Swansea City | 22 | -25 | 18 |
18 | Crystal Palace | 22 | -10 | 17 |
19 | Sunderland | 22 | -20 | 16 |
20 | Hull City | 21 | -25 |
0 comments :
Post a Comment