Na.Alex Mathias.
Mabingwa watetezi wa Kombe la Azam
Sport Federation ‘FA’ imeanza vyema kutetea taji hilo kwa mara ya pili
baada ya kupata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Ashanti United mchezo
uliochezwa katika uwanja Uhuru jijini Dar es salaam.
Yanga walikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya 20 likifungwa na Mshambuliaji Amis Tambwe akipokea pasi safi toka kwa winga hatari Simon Msuva kuingia kwa bao hilo liliwachanganya Ashanti ambao walikuwa wanatumia mchezo wa kujilinda.
Mchezaji mwenye kucheza nafasi mbili za kiungo cha juu na kati,Thabani Kamusoko
kufunga la pili dakika ya 37 baada ya kuachia bonge la shuti mita 20 na
kumuacha Mlinda mlango hana cha kufanya hadi Mapumziko Yanga walikuwa
mbele.
Kipindi cha pili Simon Msuva
alipachika bao la tatu kwa njia ya penati dakika ya 53 baada ya
kuchezewa rafu ndani ya box na katika dakika ya 60 Ashanti United
walipata bao la kuvutia machzi kupitia kwa Isaac Hassani akitumia makosa
ya beki Dante.
Yussuph Mhilu akitokea benchi aliifungia bao la nne akipokea kazi nzuri ya Emmanuel Martin na kwa matokeo hayo Yanga wamesonga mbele kwa jumla ya magoli 4-1 na watapangiwa na timu nyingi zitakazofuzu.
Katika uwanja huo Wekundu wa
Msimbazi Simba watashuka kesho Jumapili kucheza na timu ya Daraja la
pili Polisi Dar es salaam kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es salaam.
0 comments :
Post a Comment