Waziri
Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa,
amesema kasi ya kuimarika kwa umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya
upinzani nchini, kunaitia kiwewe CCM kiasi cha kuanzisha mbinu chafu za
kisiasa.
Kauli
hiyo aliitoa jana mjini Kahama katika Hoteli ya Gaprina ambapo alifikia
kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Kagera katika ziara ya
kuimarisha chama chake.
Alisema
kuimarika kwa mshikamano huo chini ya mwavuli wa Vyama Vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ni hatua kubwa katika kuelekea
kuing’oa CCM.
“Wameanza
mbinu zao za kutaka kutuondoa katika umoja wetu, wameanza kuwalisha
viongozi wetu maneno, mfano gazeti (nalitaja jina) la leo (jana)
wamenilisha maneno ya kwamba eti nimeitabiria CCM ushindi katika
uchaguzi mdogo wa udiwani kule Arumeru.
“…
mambo ya ajabu kabisa hili gazeti linaishi kwa kodi zetu sisi wananchi
leo linaamua kutumika kuvunja demokrasia inasikitisha sana.
“Wanaandika
uongo mchana kweupe kuwa nilikuwa katika kampeni kwenye kitongoji
Ematasia..mimi sikwenda huko..lakini mbinu zao hizi wananchi
wameshazijua na hawako tayari kuona hamu yao ya kupata mabadiliko
inapotea,” alisisitiza.
Wakati
huo huo mamia ya wakaazi wa mji wa Kahama waliizingira Hoteli ya
Gaprina alikofikia Lowassa, wakiwa na nia ya kutaka kumwona.
Akiwa
njiani kuelekea Bukoba, Lowassa na msafara wake alipata nafasi ya
kusalimiana na wananchi katika mnada wa Lusaunga wilayani Biharamlo,
ambako wananchi hao walimwambia kuwa hali yao ya maisha ni ngumu pamoja
na hali mbaya ya ukame inayowakabili.
Hata
hivyo Lowassa hakutoa kauli yoyote kwao zaidi ya kusema kwa sasa
mikutano ya hadhara imepigwa marufuku na asingependa kuvunja sheria kwa
kile alichodai amri kandamizi.



0 comments :
Post a Comment