Moto
mkubwa umezuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa
leo na kusababisha taharuki kubwa kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja
huo, ambapo imelazimu shughuli zote uwanjani hapo kusitishwa kwa muda
wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea na kazi yao kwenye uwanja huo
mkubwa zaidi nchini Tanzania.
Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno amesema kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za kawaida zinaendelea kama kawaida.
Aidha
Meneja wa Uwanja huo ameeleza kuwa kwa sasa shughuli zote za
usafirishaji zimeamishiwa Terminal One na zinaendelea kama kawaida huku
wakiweka sawa maeneo yalioathirika.
“Kwanza
naomba niwatoe hofu Watanzania na wasafiri wote wanaotumia Uwanja wetu,
ni kweli moto umezuka kuanzia majira ya saa 6 hadi saa 7 usiku wa
kuamkia leo.
“Lakini
madhara kidogo yametokea kwenye jengo la kuhifadhia mizigo pekee,
hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na moto, mashine
zote zipo salama na sasa shughuli zote za usafirishaji tumezihamishia
kule terminal one (Uwanja wa zamani) zinaendelea kama kawaida”. Amesema
Meneja huyo.
“Baada
ya kuudhibiti moto huo tumerudi kuangalia chanzo tukakuta, mfumo wa
umeme uko sawa, hivyo hatujajua chanzo hasa cha moto huo ila
tunajitahidi kufanya utafiti ili tujue.” Aliongeza Meneja na kusema
taarifa zaidi, zitatolewa baadaye.
Chanzo: GPL







0 comments :
Post a Comment