Mahakama
moja ya New York Marekani imeridhia ombi la wanaharakati waliokwenda
Mahakamani kupinga amri ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo, kupiga
marufuku Wakimbizi wa Syria na raia wengine wa nchi sita za kiislamu
kama Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen wasiingie Marekani.
Mahakama
hiyo imeamuru wote waliozuiliwa kupitia amri hizo waachiwe ikiwa ni
agizo la lililotolewa saa kadhaa baada ya kuwepo Ripoti kutoka uwanja wa
ndege wa John F Kennedy New York kwamba watu kadhaa wamezuiwa kuingia
Marekani wakiwemo wale ambao walikuwa wamepewa ruhusa kwenda kuishi
Marekani kupitia mpango maarufu wa Green Card.
Tayari
pia Raia wawili wa Iraq wameishitaki Mahakamani serikali ya Marekani
baada ya kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa John F. Kennedy New York
na kuzuiwa kuingia Marekani ambapo inaripotiwa wakati huo kuna raia
wengine 10 walikua wamezuiwa kuingia Marekani muda mfupi tu baada ya
ndege kutua.
0 comments :
Post a Comment