Makamu wa Rais Gambia ajiuzulu


Isatou Njie, Makamu wa Rais wa Gambia
 
ISATOU Njie, Makamu wa Rais wa Gambia ametangaza wazi kuachia ngazi hiyo kufuatia sintofahamu ya hali ya kisiasa iliyotanda katika Taifa hilo la Afrika Magharibi, anaandika Wolfram Mwalongo.
Hatu hiyo imekuja wakati tayari Mawaziri zaidi ya saba wamejiuzulu, hali hiyo imetokana na uamzi wa Rais Yahya Jammeh kutangaza wazi kwamba hawezi kuachia nchi kwa mpinzani wake Adama Barroa aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Rais Jammeh amekataa katu kuondoka Ikulu ya nchi hiyo kwakile alichodai kwamba uchaguzi uliompa ushindi mpinzani wake uligubikwa na kasoro hivyo anataka urudiwe.
Bunge la nchi hiyo limetangaza kumwongezea muda kiongozi huyo huku Wafuasi wa Barrow wakishutumu maamzi hayo kwa kile wanachodai bunge la nchi hiyo limeshindwa kusimami misingi ya sheria.
Kwa mjibu wa Shirika la habari la Al Aljazeera Adama Barrow ambaye alipaswa kuingia Ikulu ya Gambia hii Jana, anatarajiwa kuapishwa ubalozini nchini Senegal.
Wakati huo vikosi vya kijeshi kutoka mataifa mbalimbali ya  Jumuhiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi (ECOWAS) vimeendelea kutia nanga kwenye Ardhi ya Gambia ikiwa ni maandalizi ya kumung’oa kwa mtutu Rais Jammeh.
Ousman Badjie Mkuu wa majeshi wa Gambia hivi sasa ameonekana kujiweka kando na Rais Jammeh kwakile alichodai kuwa hatathubutu kuruhusu majeshi yake kufanya mashambulizi kwa yeyote.
Huku akionekana kubadili msimamo wake wa awali ambapo Jenerali huyo alitangaza wazi kumuunga mkono Rais aliyemadarakani.
Wagambia wameendelea kukimbia nchi yao na kuingia nchini Senegal kwakuhofia machafuko kutokana na azma ya Wafuasi wa Barrow kumtangaza Rais Jammeh kuwa “muasi”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment