Timu ya Manchester United imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kushinda mechi ya sita mfululizo Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kung’ara ugenini dhidi ya wenyeji West Ham kulala 2-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Olympic Stadium mjini London.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa kocha Jose Mourinho licha ya wenyeji kuwa pungufu hadi mapumziko timu hizo zilikwenda sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Man United waliweza kupata kunufaika kwani dakika ya 63 Juan Mata alifunga goli la kwanza na 78 mkongwe Zlatan Ibrahimovic akifunga la pili huku likiwa ni la 13 kwenye orodha ya wafungaji huku kinara akiwa ni Diego Costa mwenye magoli 14.
Kwa Matokeo hayo Manchester United wamebaki katika nafasi ya 6 licha ya kufunga wakiwa na pointi 39 na kinara wa msimamo akiwa bado Chelsea anaongoza akiwa na pointi 49.
VIKOSI:WEST HAM (4-3-3): Randolph; Nordtveit, Reid, Ogbonna, Cresswell; Feghouli, Kouyate (Fernandes 82mins), Obiang; Lanzini (Ayew 89), Payet (Carroll 69), Antonio
Subs not used: Adrian, Quina, Fletcher, Noble
Sent off: Feghouli 15
Booked: Payet, Nordtveit
MANCHESTER UNITED (4-3-3): De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian (Mata 46), Carrick, Herrera, Pogba, Lingard (Rashford 58), Mkhitaryan (Smalling 65), Ibrahimovic
Subs not used: Romero, Fellaini, Young, Martial
Goals: Mata 63, Ibrahimovic 78
Booked: Darmian, Valencia
0 comments :
Post a Comment