Mkuu wa mko wa Rukwa kamishna
Mstaafu Zelote Stephen amewaagiza wakuu wa Wilaya kutokubali kupokea
mifugo kutoka katika wilaya nyingine bila ya mifugo hiyo kuipa kibali
maalum cha kuhamia katika wilaya zao.
Ameyasema hayo katika amri halali
namba 1/2017 kuhusu kupokea, kuingiza, kuihamisha, kusafirisha na
kupitisha mifugo ndani ya mkoa wa rukwa kwa mamlaka aliyopewa na kifungu
cha 7 cha sheria Nambari 19 ya mwaka 1997 ya Tawala za Mikoa Sura Namba
97 mapitio ya mwaka 2002, kwa lengo la kusimamia na kutekeleza maagizo
ya waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2002 unaokataza kabisa usafirihaji
kiholela wa mifugo.
“Mifugo isihamishwe kutoka katika
Kijiji, Wilaya ama Mkoa kabla ya kupata kibali cha Kijiji, Wilaya ama
Mkoa inakopelekwa. Hivyo Kijiji, Wilaya na Mkoa itatoa kwanza idhini ya
kupokea mifugo hiyo ndipo kibali cha kusafirisha mifugo kitolewe,”
Zelote Stephen alisema.
Zelote Stephen alisisitiza kuwa
Vijiji, Wilaya na Mkoa usitoe vibali vya kupokea mifugo kabla ya
kujiridhisha kwamba wanayo maeneo ya kutosha ya malisho ya mifugo,
yaliyopimwa na kuthibitishwa na wataalamu kama yanafaa kwa malisho na
maji ya kutosha na majosho ya kuoshea mifugo.
Vile vile Mkuu wa Mkoa aliwaagiga
maafisa mifugo kuanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya na Mkoa kusisimamia na
kuhakikisha hakuna mifugo inayosafirishwa kutoka Kijiji, Wilaya na Mkoa
kwenda Mkoa mwingine au kuingia katika Kijiji, Wilaya au Mkoa bila ya
kupimwa na kuchanjwa chanjo lengo likiwa ni kuthibiti uenezaji wa
magonjwa ya mifugo nchini.
“Kabla ya kutoa vibali vya
kusafirisha mifugo, madaktari wa mifugo wa Wilaya ama wawakilishi wao
wahakikishe kwamba mifugo inaogeshwa na kuchanjwa dawa za kuzuia
magonjwa husika kabla ya kuiruhusu mifugo hiyo kusafirishwa ili kuzuia
uenezaji wa magonjwa ya mifugo,” Zelote Stephen alifafanua.
Aidha Mkuu wa Mkoa
amewatahadharisha maafisa mifugo ambao sio waaminifu wanaotumia njia ya
kuingiza mifugo kwenye wilaya kwa njia ya biashara za minada na matokeo
yake mifugo hiyo kubaki eneo husika bila ya kufuata taratibu zozote.
Amri hii itafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 9 January, 2017 hadi tarehe 31 Desemba, 2017.
0 comments :
Post a Comment