Na.Alex Mathias.
Ushindi wa tatu wa Simba katika
Michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar yameifanya ifikishe jumla ya
pointi 10 na kuongoza kundi A na sasa itakutana na watani wao jadi Yanga
Mchezo wa Nusu Fainali itakayopigwa siku ya Jumanne kwenye uwanja wa
Amaan baada ya kuwatandika Jang’ombe boys magoli 2-0.
Simba waliuanza mchezo kwa kasi ya 4G huku Shiva Kichuya akiwatesa mabeki wa Jang’ombe boys na katika dakika ya 11 Laudit Mavugo aliwanyanyua mashabiki waliokuwa wamefurika akimalizia kazi nzuri ya Kichuya na mashabiki kulipuka shangwe kwa kusema kuwa tunaitaka Yanga Nusu fainali.
Hadi mwamuzi Mfaume Nassoro
anapuliza kipyenga cha Mapumziko Simba walikuwa mbele kwa ushindi wa
bao hilo moja la mshambuliaji Raia wa Burundi ambaye amekuwa kwenye
wakati mgumu kutokana na kushindwa kuonesha kiwango cha hali ya juu kwa
mashabiki wa Simba.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote kufanya mabadiliko hata hivyo Simba waliendelea kuumiliki mchezo
huo na kuweza kupata bao la pili dakika ya 53 kupitia kwa Laudit Mavugo
aliyeachia bonge la shuti na kujaa moja kwa moja golini huku shangwe za
mashabiki wa Simba zikisema kiama kwa Yanga siku ya Jumanne ya Januari
10.
Hadi dakika 90 za mwamuzi Mfaume
Nassoro ubao ulikuwa ukisomeka Simba 2-0 dhidi ya Jang’ombe boys
iliyokuwa chini ya Mchezaji wa zamani wa Yanga Abdi Kassim na kuwafanya
Jang’ombe wayaage mashindano hayo wakiwa na pointi zao 6.
Kwa matokeo hayo Simba itacheza na
Yanga siku ya Jumanne saa mbili usiku mchezo wa Nusu Fainali ambao
unategemewa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na historia ya ikumbukwe
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu hizo
zilitoka sare ya kufungana 1-1.
Yanga wanaingia Nusu Fainali na
kumbukumbu ya kuunganisha kifurushi cha 4G toka kwa matajiri wa jij la
Dar es salaam timu ya Azam FC ambao waliwadhalilisha kwa kipigo cha
magoli 4-0 na tayari kamati ya mashindano imetaja viingilio vya mechi
hiyo huku kiingilio cha chini kabisa ni cha sh elfu tatu na cha juu elfu
kumi.
Mchezo wa pili utachezwa saa mbili
na robo kati ya Taifa Jang’ombe dhidi ya Mabingwa watetezi URA toka
Uganda na mshindi wa hapa atakutana na Azam FC Nusu Fainali ya kombe la
Mapinduzi.
0 comments :
Post a Comment