Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Gabriel Dangalo, amewaagiza wataalamu wa mifugo
na kilimo katika wilaya zote za mkoa wa Arusha, kuhakikisha wanafanya
sensa ya kutambua idadi ya mifugo na kuivalisha hereni.
Dangalo
ametoa kauli hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuboresha ng’ombe wa maziwa ADGG,
uliowahusisha wafugaji kutoka halmashauri ya Arusha na jiji la Arusha
iliyofanyika mkoani hapa.
Amesema
maelekezo ya mkoa ni kuhakikisha ng’ombe wote waliopo kwenye wilaya,
mkoani hapa, wanaingizwa kwenye mpango wa utambuzi kwa kuvalishwa
hereni, chini ya mradi wa kuboresha mradi wa ng’ombe za maziwa wa ADGG.
Mratibu
wa mradi huo Dk. Eliaman Lyatuu amesema suala la uwekeji hereni za
kitaifa kwa ng’ombe wa maziwa kwa ajili ya utambuzi ni mpango mzuri
ambao unafanyika kwa nchi mbalimbali duniani na tayari halmashauri ya
Arusha na jiji la Arusha, wameshavalisha ng’ombe wa maziwa zaidi ya 300 .
Ameongeza
kuwa mpango huo umepokelewa vizuri na wafugaji na utawasaidia kutambua
ng’ombe wao hata pale watakapokuwa wanahamisha mifugo kutoka eneo moja
kwenda eneo lingine, pia ng’ombe anapopotea ama kuibiwa inakuwa rahisi
kumtambua.
0 comments :
Post a Comment