Taarifa ambazo mtandao wa Global Publishers imezinyaka kutoka Mkoani Tabora, ni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Gabriel Mnyele ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kwa hiyari yake mwenyewe.
Kwa mujibu wa habari hizo, imebainika kuwa, DC Mnyele alitumia wasaha wa kuwaaga makada wa Chama cha Mapinduzi ambao walikuwa na mkutano wa kawaida hasa Madiwani wa chama hicho ambao walikuwa wakijiandaa na kikao cha Baraza.
Taarifa hizo, zimebainisha kuwa, DC huyo alimuomba Rais John Pombe Magufuli kuwa anaachana na nafasi hiyo kwa ajili ya kwenda kufanya majukumu yake mengine.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHER
0 comments :
Post a Comment