Mwanasheria amtoroka Jammeh

Edward Anthony, Mwanasheria wa Rais Yahya Jammeh nchini Gambia

Edward Anthony Mwanasheria wa Rais Yahya Jammeh nchini Gambia akimbilia uhamishoni katika taifa jirani la Senegal, anaandika Wolfram Mwalongo.
Antony ambaye amekuwa bega kwa bega katika harakati za kufungua kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa mpinzani Adama Barrow amemtelekeza mteja wake.
Hatua ya kuhamisha makazi gafla kwa Mwasheria huyo kumetokana na kupuuzwa kwa ushauri wake kwa Rais Jammeh.
Hofu na vitisho vya machafuko vimemwondoa Gambia.Rais Jammeh hajaridhia kuondoka madarakani licha ya kukaa Ikulu kwa miaka 22 sasa.
Katika barua yake ya Januari 17 (juzi) kwa Rais Jammeh, Mwanasheria huyo alimtaka kiongozi huyo kuepusha machafuko kwakukabidhi madaraka kwa mpinzani ambaye ndiye aliyetangazwa kuwa mshindi.
Hata hivyo Rais Jammeh amekuwa na moyo mugumu kusikiliza washauli mbalimbali walio anza kumsihi akabidhi nchi kwa Barrow.Kutokana na kuhofia machafuko.
Rais Jammeh alipaswa kuachia ngazi rasmi hii leo ingawa ameonesha wazi azma ya kung’ang’ana Ikulu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment