Na: Frank Shija - MAELEZO.
Rais
wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kumfutia usajili mwekezaji wa
Kiwanda cha Nyama, Kampuni ya Triple S na badala yake watafute mwekezaji
mwingine.
Agizo
hilo limetolewa leo Mjini Shinyanga wakati akiwahutubia wananchi wa mji
wa huo ambapo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi iliyoambatana na
sherehe ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
“Futeni
usajili wa mradi wa Triple S, haiwezekani mwekezaji akashindwa
kuendesha kiwanda kwa zaidi ya miaka 10 sasa afu tuendelee kumkumbatia,
tafuteni mwekezaji mwingine, mkishindwa semeni Serikali iweke hela, ili
uzalishaji uendelee,” alisisitiza Rais Magufuli.
Aliongeza
kuwa mwekezaji huyo amekuwa mbabaishaji kwani tangu kipindi yeye (Rais
Magufuli) alipokuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo alimfahamu na alimpa
maelekezo cha kusikitisha hakuna jambo aliloendeleza ikiwemo kuanza kwa
uzalishaji.
Akizungumzia
sababu ya kufanya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar katika upande
huu wa Bara Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni moja, na kuongeza
kuwa chimbuko halisi la uwepo wa Taifa la Tanzania ni Mapinduzi ya
Zanzibara mabapo miezi michache tu baada ya kufanyika kwa mapinduzi hayo
Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaliwa kwa Taifa la Tanzania.
Kwa
upande wake Waziri wa TAMISEMI na Kazi maalumu kutoka Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri amesema wao kama Wazanzibar
wamefarijika sana kwa kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuamua
kushiriki maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu kwa kusherehekea katika
upande wa Bara kitu ambacho akijawahi kufanyika kabla.
Aliongeza
kuwa ujio wake umetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi moja hivyo
Rais Magufuli alivyoeleza nia yake ya kuadhimisha Maapinduzi huku Bara,
Rais Dkt. Shein alimteua aje kumwakilisha na kueleza kuwa maefarijika
sana na kusema Tanzania ni yetu sote na tutaendelea kuwa wamoja.
Rais
Dkt. Magufuli yuko ziarani Mkoani Shinyanga ambapo kesho anatarajiwa
kufungua viwanda kadhaa vilivyopo mkoani hapo, baadhi ya viwanda hivyo
ni pamoja na Kiwanda cha Vinywaji Baridi (maji) cha Jambo, Kiwanda cha
Mafuta na vingene.



0 comments :
Post a Comment