Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad,
amemwandikia barua Gavana wa Benki ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu
ili achukue hatua za kulishughulikia sakata la fedha za ruzuku
zinazodaiwa kukwapuliwa na CUF upande wa Mwenyekiti anaetambuliwa na
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.
Maalim
Seif ameandika barua hiyo yenye kumbukumbu namaba CUF/HQ/AKM/003/017/01
na nakala zingine kuzituma kwa mamlaka mbalimbali.
Katika
barua hiyo kwa Profesa Ndulu, Maalim ameamabatanisha kumbukumbu ya
miamala ya fedha ilivyofanyika, pia amesema kuwa chama hicho kinaendelea
na taratibu za kukamilisha hatua za kisheria ili kuwafikisha mahakamani
wahusika wote walioshiriki katika kuchukua fedha hizo, akiwapo Msajili
wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi.
Amesema
kuwa, Mutungi atakuwa na kesi ya pili na atashtakiwa kutokana na madai
ya kushirikiana na walalamikiwa wale wale wa kufungua akaunti mpya ili
wapewe ruzuku.
Aidha,
amesema Jaji Mutungi amefanya hivyo huku akifahamu fika kuwa kuna kesi
ya msingi iliyopangwa kusikilizwa Februari 2, 2017 mbele ya Jaji Kihiyo.
“Gavana
baada ya Muhtasari huo, kwa masikitiko makubwa leo nakuandikia barua
hii kukujulisha kuwa njama za kuiba fedha za ruzuku ya CUF Chama cha
Wananchi zimefanikiwa kwa kufanya muamala wa jumla ya shilingi
369,378,502.64 toka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwenda akaunti
namba 2072300456 ya NMB tawi la Temeke januari 5 mwaka huu,”amesema
Maalim.
Hata
hivyo, hivi karibuni CUF upande wa Maalim Seif ulilalamikia hatua
iliyochukuliwa na Jaji Mutungi kuwapa CUF upande wa Profesa Lipumba
zaidi ya shilingi milioni 360 za ruzuku
0 comments :
Post a Comment