WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema jumla ya vijiji 53 vya mkoa wa Njombe
vitapatiwa huduma ya maji safi na salama katika mwaka huu wa fedha.
Alitoa
kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizungumza na
wananchi wa wilaya ya Wanging’ombe katika mkutano wa hadhara katika kata
ya Ilembula.
Waziri
Mkuu alisema zaidi ya sh. bilioni 2.4 zimetengwa kwa ajili ya
kugharamia mradi huo wa maji katika miji ya Makambako, Njombe na wilaya
ya Wanging’ombe.Alisema kati ya vijiji hivyo vitakavyopatiwa maji,
vijiji 22 ni vya wilaya ya Wanging’ombe, hivyo aliwaomba wananchi hao
kuwa na subira.
Kwa
mujibu wa Waziri Mkuu tayari zabuni ya mradi huo imeshatangazwa, hivyo
amewaagiza viongozi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji watafute mkandarasi
mzuri.Alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kila
mwananchi anapata huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka
mahali anapoishi.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa Wanging’ombe, Mheshimiwa
Mhandisi Gerson Lwenge kumuomba awasaidie katika kutatua kero ya
maji.Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji alisema
“Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi tunakabiliwa na changamoto ya maji, leo
tunaomba ututatulie kero hii”.
Changamoto
nyingine aliyoitaja Mheshimiwa Lwenge ni pamoja na ukosefu wa hospitali
ya wilaya, ambapo Waziri Mkuu aliigiza halmashauri hiyo kuanza
ujenzi.Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 inaelekeza
kuwa na hospitali katika kila wilaya, kituo cha afya kwa kila kata na
zahanati kwa kila kijiji.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Ally
Kasinge kukutana na viongozi wa kata na vijiji vinavyozunguka hifadhi ya
Mapanga Kipengele ili kutatua kero ya mpaka.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
0 comments :
Post a Comment