Timu ya Senegal imeanza vyema
katika michuano ya kombe la Mataifa barani Afrika ‘AFCON’ baada ya
kuilaza Tunisia jumla ya magoli 2-0 mchezo uwanja wa Stade de
Franceville mjini Franceville nchini Gabon.
Magoli mawili ya Senegal
yameifanya iwe timu ya kwanza kupata pointi tatu muhimu baada ya
kushudia kundi A timu zikitoka sare hivyo Simba watelanga wameongoza
kundi B huku Algeria na Zimbabwe zikitoka sare ya kufunga magoli 2-2.
Alikuwa mshambulizi wa Liverpool Saido Mane alianza kuwa nyanyua washabiki wa Senegal dakika ya 10 kwa njia ya penati baada ya Nahodha Cheikhou Kouyate kuangusha ndani ya box na dakika ya 30 beki Kara Mbodj alifunga goli la pili akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Balde Diao Keita na kuwazidi ujanja wachezaji wa Tunisia.
Licha ya kufungwa magoli hayo
mawili Tunisia waliedelea kuwapeleka Mchakamcha Wasenegal hao hadi timu
zinaenda mapumziko wageni kwenye ubao walikuwa mbele kwa magoli mawili.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote mbili kufanya mabadiliko hata hivyo hakuna aliyeweza kupata goli
kipindi hicho Mpaka mwamuzi anapuliza kipyega Senegal wameibuka na
ushindi wa magoli 2-0 na kuwafanya wawe vinara wa kundi B.
Michuano hiyo inaendelea tena Leo
kwa michezo miwili kupigwa mchezo wa kwanza utakuwa majira ya saa moja
kamili kwa saa za Afrika Mashariki kati ya Ivory Coast dhidi ya beki wa
Yanga Vicent Bossou timu ya Togo na mchezo wa pili utakuwa kati ya
D.R.Congo dhidi ya Morocco.


0 comments :
Post a Comment