Mtazania Alphonce Simbu akimalizia mbio za Mumbai Marathon baada ya kuongoza na kwakuwashinda wapinzania wake katika mbio hizo.
Mtazania Alphonce Simbu wa pili
kutoka kushoto akiwa na washindi wenzake waliomfuatia mara baada ya
kumalizia mbio hizoza Mumbai Marathon akiwa mshindi wa kwanza
Mtazania Alphonce Simbu
akionyesha medali yake ya dhahabu aliyojishindia katika mbio za Mumbai
Marathon baada ya kuongoza na kwashinda wapinzania wake katika mbio
hizo.
………………………………………………………………………………….
• Awatimulia vumbi Wakenya, Waethiopia.
• Asema ni Ushindi wa Watanzania
Mtazania Alphonce Simbu, ameibuka mshindi wa mashindano ya
Mumbai Marathon ya mwaka huu huku akimtimulia vumbi Mkenya Joshua
Kipkorir katika kundi la wakimbiaji wa nje. Mtanzania huyo aliongoza
huku akifuatiwa na Wakenya 7 na Waethiopia 2 katika 10 bora.
Mashindano hayo yajulikanayo kama Standard Chartered Mumbai
Marathon yanafanyika kila Jumapili ya tatu ya mwezi Januari katika jiji
la Mumbai nchini India na ni mbio zinazoaminika kuwa kubwa kabisa barani
Asia kwa idadi ya washiriki wanaomaliza.
Simbu, ambaye anadhaminiwa na kampuni ya Multichoice Tanzania,
aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa 2:09:28 muda ambao ni mzuri sana
kwa mbio za aina hiyo.
Akizungumzia ushindi wake, Simbu amesema kuwa anaamini ushindi
huo umesababishwa na maandalizi aliyoyafanya na kwamba udhamini wa
kampuni ya Multichoice Tanzania umemsaidia sana kwani imekuwa rahisi
yeye kutumia muda mwingi zaidi kwenye mazoezi na maandalizi.
Amesema anauchukulia ushindi huo kama changamoto kwa mashindano
mengine makubwa na kwamba huo ni mwanzo tu. Amesisitiza kuwa ushindi huo
siyo wake peke yake au Multichoice , bali ni ushindi wa Taifa zima la
Tanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Mahusiano wa Multichoice Tanzania
Johnson Mshana amesema Multichoice imefurahishwa sana na matokeo hayo na
kwamba wataendela kumdhamini Simbu kwa mujibu wa makubaliano yao, ili
kuhakikisha anaendelea kufanya vyema na kuliletea taifa sifa kubwa.
“Tulichukua jukumu la kumdhamini simbu katika mazoezi na
maandalizi yake kwa kipindi cha mwaka mzima, kwani tunafahamu fika kuwa
mazoezi na maandalizi ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika mchezo
wowote. Alisema Mshana na kuongeza “dhamira yetu kubwa ni kuinua vipaji
na kulirejesha taifa letu kwenye ramani ya dunia katika ulingo wa
michezo na burudani”
Katika mbio hizo, waigizaji maarufu wa .Bollywood John Abraham and Neha Dhupia walikuwepo kuleta amsha amsha kwa washiriki.


0 comments :
Post a Comment