SIKU moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua
hatamu ya uongozi wa taifa hilo amewashutumu waandishi wa habari akiwaita watu waongo zaidi dunuiani.
Trump ametoa kauli hiyo akionekanwa kukerwa na taarifa juu ya idadi ya watu waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake.
Wakati vyombo vya habari vikisema idadi ya watu waliohudhuria ni 250,000 kinyume na 900,000 waliokadiria awali, Trump anadai watu milioni 1.5 walihudhuria sherehe hiyo.
Idadi hiyo ni ndogo kulinganisha na watu milionin 1.9 waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama mwkaa 2008.
Msemaji wa White House, Sean Spicer, amesema vyombo vya habari vinaendesha kampeini ya kugawa watu kwa kuangazia habari ambazo hazina msingi wowote.
Hata hivyo, kanda za video za matangazo ya moja kwa moja wakati wa hafla hiyo hazikunasa umati mkubwa wa watu kama anaodai Trump.
Picha zinaonekana zikionyesha watu wengi zaidi waliohudhuria shereha ya kupishwa kwa Rais Barack Obama mwaka 2009.
Trump hakuzungumzia maandamano ya watu wanaompinga wakati akitembelea Makao Makuu ya Shirika la Ujasusi Marekani (CIA) katika Jimbo la Virginia juzi, badala yake alivishambulia vyombo vya habari.
Trump alisema kuwa video na picha wakati wa kuapishwa kwake zilionyesha taarifa ziziso za ukweli.
“Walionekana watu kama milioni 1.5 siku ya Ijumaa, alisema Trump, akipinga ripoti za vyombo vya habari kuwa walikuwa watu chini ya 250,000.
“Ndio maana nasisitiza kwamba waandishi wa habari ni watu waongo zaidi duniani.”
0 comments :
Post a Comment