Kiongozi
Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewataka marais wastaafu
kutokaa kimya, badala yake wajitokeze kumshauri rais Magufuli wanapoona
mambo hayaendi sawa ili kunusuru nchi na uchumi.
Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Isagehe, Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
“Hii
nchi inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia, nawaomba marais wastaafu
wasikae kimya kuhusu kunusuru nchi, wamshauri rais kuhusu mambo
mbalimbali likiwemo la vyama vya siasa kuzuiwa kufanya mikutano ya
hadhara,”amesema Zitto.
Aidha,
Zitto amemuomba rais Magufuli kufanya mabadiliko katika sekta ya madini
kwa kuweka wazi mikataba ya wawekezaji na kwamba jambo hilo litasaidia
wananchi kuwa na uelewa wa mikataba hiyo.
Hata
hivyo, Zitto ameshangazwa kuona barabara inayounganisha migodi mitatu
ya dhahabu ya Buzwagi, Bulyanhulu na Geita Gold Mine kuwa barabara hiyo
haina kiwango cha lami.
0 comments :
Post a Comment