Mataifa ya Amerika yamekuwa kwenye vita dhidi ya biashara hiyo haramu iliyoshamiri huku ikiendeshwa na mitandao hatari ya matajiri.Kumnasa El Chapo na hatimaye kumsafirisha nchini Marekani kumeongeza matumaini katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika bara la America kwani El Chapo alikuwa kiongozi wa genge maarufu la Sinaloa nchini Mexico.
Genge la El Chapo lilikuwa likiuza dawa za kulevya nchini Mexico na katika mataifa jirani ikiwemo Marekani, Argentina na Brazil jambo lililosababisha Marekani kumsaka kumtangaza kama mtu hatari anayesakwa kwa udi na uvumba.
Marekani ilikuwa ikimuwinda mfanyabiashara huyo hususan baada ya kutoroka gerezani mara mbili nchini Mexico akitumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kuchimba handaki liloingia gerezani na kumtorosha. Njama iliyosukwa na wasaidizi wake.
El Chapo pia alitoroka kupitia bomba lenye urefu wa kilometa 1.5 kupitia gerezani huku njama za kumtorosha zikidaiwa kusukwa na vigogo wa gereza kwa lengo la kumnusuru asipelekwe nchini Marekani.
Kabla ya kupelekwa Marekani wiki hii, mfanyabiashara huyo alikata rufaa mara kadhaa akipinga kupelekwa ugenini lakini hoja zake zikapuuzw na sasa yupo mikononi mwa Marekani na huenda ikawa ndiyo mwisho wa matukio yake ya kutoroka.
0 comments :
Post a Comment