Na: Jovina Bujulu – MAELEZO
SERIKALI mkoani Iringa imesema
hakuna njaa kwa sababu msimu wa mwaka 2015/2016 walizalisha tani zaidi
ya milioni 1.4 zikijumuisha mazao ya nafaka, mizizi na mazao jamii ya
kunde.
Akizungumzia hali ya upatikanaji
wa chakula mkoani humo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa
baadhi ya wananchi wengi wamejawa na tamaa ndiyo maana wanauza chakula
badala ya kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya familia zao.
“Kila kaya inatakiwa kuhakikisha
ina chakula cha kutosha badala ya kukiuza, na wataalam wa chakula
wataendelea kupita kila nyumba kuhimiza utuinzaji wa chakula sambamba na
uwiano wa mahitaji halisi,” alisema Mama Masenza.
Aliongeza kuwa kwa sasa Mkoa huo una ziada ya mazao ya nafaka tani 756,369.92 na kunde tani 61,584.63.
Hata hivyo alitoa wito kwa baadhi
ya wananchi kuthamini familia zao kwa kuhifadhi chakula badala ya
kukiuza kwa tama zao za kupata fedha kirahisi.
0 comments :
Post a Comment