Mwenyekiti
wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashim Rungwe, amemtembelea
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), ambaye bado yuko
mahabusu katika Gereza la Kisongo mkoani Arusha.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Arusha jana baada ya kuonana na mbunge
huyo, Rungwe alisema baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye jamii
yanasababishwa na baadhi ya watawala.
Alisema hali hiyo imekuwa ikiibua chuki miongoni mwa wananchi jambo ambalo si zuri na linahitaji kukemewa.
Kiongozi
huyo alimtembelea Lema akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali
akiwamo Makamu Mwenyekiti wa Chauma, Kayumbo Kabutali na wabunge wa
Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare na Moshi Vijijini, Antony Komu, wote wa
Chadema
“Historia
ya zamani inatufunza matatizo yanayotokea katika jamii yanachangiwa na
mambo yanayotendwa na baadhi ya watawala ambayo yanaleta chuki.
“Na chuki siyo kitu kizuri kwa sababu inazidi kuwa kubwa kwenye mioyo ya watu hata kama wako kimya,”alisema na kuongeza:
“Hili
limewahi kutokea enzi za mitume hata Nelson Mandela aliwekwa ndani na
alipotoka dunia nzima iliamka hivyo tunaona kuna baadhi ya watu
wanawekwa ndani bila sababu ya msingi, natoa wito kwa wenye mamlaka
kuangalia suala hili.”
Mwenyekiti
huyo alisema ni wakati wa watanzania wote kwa ujumla kupigia kelele
suala hilo kwa vile Mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi, anazuiliwa
kwa makosa yenye dhamana jambo la kukemewa.
“Tumekuja
Arusha kumuangalia Lema kwa sababu ni mwenzetu na tuna masikitiko na
kama walifikiri wakimuweka Lema ndani wanamsimamisha au kumkomesha,
wanamkomaza kisiasa.
“Anapata ujasiri wa aina Fulani kwa sababu haelewi kwa nini yuko ndani, wangemkuta na malori matatu ya silaha sawa,” alisema.
Mbunge
wa Bukoba Mjini alisema ameridhishwa na kupata matumaini na hali ya
mbunge huyo kwa vile ni yuleyule na ameongeza ujasiri wa kulisema lile
analoamini.
Naye
Mbunge wa Moshi Vijiji, Antony Komu, alisema Lema ameomba wabunge wote
bila kuangalia itikadi za vyama vyao wanapaswa kuwa makini wakati wa
utungaji wa sheria.
Alisema kutokana na baadhi ya upungufu wa sheria kuna watu wako gerezani kwa muda mrefu.
Alisema katika gereza hilo asilimia kubwa wako gerezani kwa muda mrefu kutokana na upungufu wa sheria mbalimbali.
0 comments :
Post a Comment