Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema
miongoni mwa changamoto anazokutana nazo ni pamoja kupigiwa simu za
vishawishi na wanawake hasa usiku wa manane, wakidhani anapata pesa
nyingi kwenye kazi yake.
Kamishna
Sirro amefichua siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha East
Africa Breakfast, ambapo amesema pamoja na changamoto hizo, anajitahidi
kukabiliana nazo kwa kuwa tayari amekwishawazoea.
Amesema
kuwa kuna wanawake wengine wakiona amependeza kwenye tukio fulani,
wanajua lazima atakuwa na pesa za kuwasaidia katika maisha yao hivyo
wakati mwingine humpigia simu usiku, na yeye akidhani kuwa ni taarifa za
uhalifu, lakini hukutana na vishawishi vikiambatana na sifa kedekede.
“Mwigine
anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini,
wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee
tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi”.
Amesema Kamanda Sirro
Aidha,
Sirro ametaja changamoto nyingine ambazo hukutana nazo kuwa ni pamoja
na suala la askari wake kulalamikiwa jambo linaloonesha dhahiri kama
kiongozi ameshindwa kuwasimamia vijana anaowaongoza na mara nyingi huwa
anachukua hatua.
Hata
hivyo, Lingine ni uhalifu kuzidi katika eneo fulani na hufanya wananchi
kuwa na uoga, na kupoteza imani kwa Jeshi la Polisi jambo ambalo
linamfanya yeye ajisikie vibaya zaidi kuliko hata wananchi, huku
nyingine ikiwa ni viongozi wa mitaa kutowajibika katika kudhibiti
uhalifu pamoja na kuletewa
0 comments :
Post a Comment