Kocha Julio Aiponda Yanga..Adai ni Kama Gari la Kubeba Maiti

Kocha mwenye maneno mengi ambaye hivi karibuni Jamhuri Kihwelo 'Julio' alitangaza kustaafu kufundisha mpira nchini ameibuka na kuiponda Yanga kuwa haikuwa na uwezo wa kuifunga Simba, huku akiifananisha na gari ya maiti

Julio ambaye amewahi kuichezea Simba na baadaye kuifundisha kwa nyakati tofauti, ametoa kauli hiyo mara baada ya Simba kuishushia kipigo Yanga cha mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam.

Kocha huyo ambaye alitangaza kustaafu akiwa na timu ya Mwadui FC kwa madai ya kuchoshwa na waamuzi wa Tanzania, amesema ameamua kuunganisha nguvu kutoka kwa baadhi ya wachezaji wa zamani wa Simba akiwemo Zamoyoni Mogella, kuunda kundi la hamasa kwa wachezaji wa Simba ili kuhakikiksha Simba inaifunga Yanga na kuchukukua ubingwa msimu huu.

Amesema kabla na wakati wa mchezo wa jana, yeye na wenzake wamefanya kazi kubwa ya kuwatia hamasa wachezaji na hata wakati wa mapumziko, waliingia vyumbani na kuwatia hamasa wachezaji ya kupambana na ndiyo maana timu kipindi cha pili ilibadilika na kucheza kwa ari kubwa.

"Sisi kazi yetu ni kuwahamasisha wachezaji, hatumuingilii mwalimu, mwalimu anafanya kazi yake, lakini sisi tunawaambia wachezaji wanapaswa kupambana, ndiyo kazi tuliyoamua kuifanya kuelekea mchezo huu hata wakati wa mapumziko, kwa kazi tuliyofanya Yanga wasingeweza kutufunga, na mimi tangu nimeanza kufundisha mpira sijawahi kufungwa na Yanga, .. Yanga ni kama gari ya maiti, ya kwanza kuondoka, ya mwisho kurudi, ndiyo maana nasema hawa ni kama mwembe wetu wa uwani, wakati wowote tunautikisa unadodosha maembe" Amesema Julio.

Pia Julio amewapongeza makocha wa Simba kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuusoma mchezo na kufanya mabadiliko yenye tija, pamoja na kuwajenga wachezaji kisaikolojia, ambapo licha ya kuwa nyuma, pamoja na mchezaji wao mmoja kutolewa, walionesha kutokata tamaa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment