Manji ambaye alikwenda Polisi toka Alhamisi iliyopita, leo jioni ameonekana na Waandishi wa habari nje ya kituo cha Polisi kati Dar es salaam akichukuliwa na gari la Wagonjwa aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili za DFP na kuondoka nae huku gari lake aina ya Range Rover likitangulia mbele.
Wakati Manji anachukuliwa na gari hilo la Wagonjwa hakuwa amebebwa bali alikua akitembea mwenyewe na kuingia kwenye gari hilo ambalo inaaminika limeelekea Hospitali ambapo mazingira ya kuchukuliwa kwake yanaonekana kwenye hii video hapa chini.
0 comments :
Post a Comment