Msanii
TID amefunguka na kuwaomba radhi Watanzania kutokana na tabia yake ya
kutumia dawa za kulevya kwani anaamini kuwa akiendelea kutumia dawa hizo
hatakuwa mfano bora hata kwa mtoto wake.
TID
anasema anaamini kutokana na matumizi ya dawa hizo huenda akawa
amewakwaza watu au kufanya mambo ambayo si mema katika jamii hivyo
anaomba kusamehewa kwani alikuwa akifanya kwa nguvu ya dawa za kulevya
na si yeye.
"Nimekuwa
muathirika na matumizi ya dawa za kulevya, leo sipo hapa kusema kwanini
nimeingia huku, nimekuja hapa kama kijana niliyepotea njia. Kutoka
moyoni, nimekuja kukiri kuwa nimeikosea sana familia yangu, mama yangu,
ndugu jamaa na marafiki hivyo nimekuja kuwaomba msamaha wote
niliowakwaza under influence ya dawa za kulevya" alisema TID
Mbali
na hilo TID anasema ameamua kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaan
Mhe. Paul Makonda katika vita dhidi ya madawa ya kulevya na kusema hata
kama watu wanaweza kumuona mnafiki si mbaya maana yeye, ameamua kutoka
katika matumizi ya dawa za kulevya.
"Nimesimama
hapa kama kijana shupavu, mpambanaji, mnyama. Vita hii inabidi uwe
mnyama kama Paul Makonda ili uweze kushinda, hakuna anayejua nimepitia
mangapi mpaka nimefika hapa, natangaza rasmi kujiunga kwenye vita hii"
alisema TID
0 comments :
Post a Comment