Rais wa Gambia Adama Barrow amemuachisha kazi mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Ousman Badjie.
Hatua
hiyo ya Rais Barrow imekuja kutokana na Badjie kutangaza mwezi Disemba
mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu kuwa atafuata amri ya Rais aliyepita
Yahya Jammeh ambaye alishindwa katika uchaguzi huo.
Hata
hivyo wanajeshi wa Gambia hawakuweza kutii amri kutoka kwa mkuu huyo wa
majeshi ambaye alikuwa chini ya Jammeh ambaye baada ya muda alikubali
kuachia madaraka hayo na kukimbilia nchini Equatorial Guinea.
Na
sasa Masanneh Kinteh ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Cuba anachukua
nafasi hiyo ya Badjie. Baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo, Kinteh
alitaja jambo lake la kwanza ambalo atalifanya katika jeshi lake ni
kuwafanya wajiamini ili waongeze hamasa yao.
“My
immediate priority as chief of defence staff is to bring back the
confidence in the troops to lift their morale,” amesema Kinteh.
0 comments :
Post a Comment