Kitendo
cha Mbunge wa Arusha mjini kukaa rumande kwa zaidi ya miezi minne sasa
pasipo kupatiwa dhamana kimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto
Zuberi Kabwe kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali iwajibishwe
Katika
mtandao wake wa kijamii Mh. Zitto amedai kuwa kitendo cha Mbunge huyo
ambaye ni muwakilishi wa wananchi kunyimwa dhamana ni siasa za ukomoaji
ambazo zinajenga chuki kwenye jamii na chuki huwa zinazaa visasi.
"Haitoshi
majaji kukemea Ofisi ya DPP, Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha
mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa.
Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa
makusudi dhidi ya wananchi" Ameandika Zitto Kabwe
Hata hivyo kauli hiyo ya Zitto imekuja mapema jana
baada ya majaji watatu kutoka mahakama ya rufaa kuitaka ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa serikali na DPP kuwa makini na kuwataka kuwashikilia
watu kwa misingi ya kisheria na kuongeza kuwa haipendezi na haingii
akilini mtu kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya
kumnyima haki ya dhamana.
"Mnatufanya
wanasheria wote hatuna akili na mnachafua mpaka mahakama, kwa hali ya
kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii
tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo
na imetushtua sana". Alisema Jaji Stella Mugasha.
0 comments :
Post a Comment