Mashabiki wa soka nchini Tanzania wamempigia kura nyingi mshambuliji wa klabu ya Simba Shiza Kichuya kuliko yule wa Yanga Simon Msuva baada ya kiwango kizuri ambacho kichuya amekionyesha hasa kwenye mtanange wa watani wa jadi.
Kichuya amba nyota yake ya soka na kupendwa na mashabiki ilionekana pale ambapo afunga goli kwa kona iliyopigwa moja kwa moja nayeye na kujaa kamabani hivyo mashabiki wa Simba kujawa na mahaba zaidi hasa wanapo utazama mafumo wake wa uchezaji.
Winga huyo wa klabu ya Simba na timu ya taifa Tanzania, Shiza Ramadhani Kichuya amembwaga kwa mbali nyota wa Yanga Simon Msuva katika shindano la kumchagua winga bora wa Ligi Kuu msimu huu
Shiza Kichuya ameibuka kidedea dhidi ya Simon Msuva, baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki wake kuliko winga huyo wa Yanga Simon Msuva kupitia kwenye mtandao wa Goal Tanzania
Winga huyu wa Wekundu wa msimbazi Kichuya amefanikiwa kuibuka kinara kwa kujikusanyia asilimia 67.7 ya kura zote huku Simon Msuva akiambulia asilimia 33.3 pekee
Htata hivyo zoezi hilo la kumchagua nani ni winga bora Ligi Kuu kwa msimu huu kati ya Shiza Kuchuya na Simon Msuva, lilianza tangu Jumapili iliyopita kwa mashabiki wote kupata fursa ya kupiga kura na kumchagua mkali kati ya hao nyota wawili kupitia mtandao wa Goal Tanzania



0 comments :
Post a Comment