Kimenuka:Bashe,Msukuma, Malima Washikiliwa Na Polisi Dodoma

Dodoma. Wabunge wawili na aliyekuwa naibu waziri wa fedha, Adam Malima wanahojiwa na polisi mjini hapa kwa kosa la kutaka kufanya vurugu na uchochezi katika vikao vya CCM.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibisha na kuwataja waliokamatwa kuwa ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe na Mbunge wa Geita vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma na Malima.

“Hao ndio waliokamatwa na bado tunaendelea na mahojiano na wengine bado tunaendelea kuwatafuta,”amesema Mambosasa.

Amesema  taarifa zaidi atazitoa baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment