Yanga Hoi Imeshindwa Kuifunga Zanaco Full Time


MPIRA UMEKWISHAAA
-KADI....Kipa wa Zanaco, Kola analambwa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda
-Kessy anapiga krosi safi kabisa, Martin anauwahi yeye na kipa lakini anashindwa kuunganisha vizuri
-Hadi sasa hakuna shambulizi kali kwenye kila lango


DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, Cannavaro anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Chirwa wa Zanaco na kuwa kona, inachongwa na kuwa goal kick
Dk 89 sasa, kila upande unaonekana uko makini katika ulinzi na Yanga wanatumia mipira mirefu zaidi ambayo inaonekana haina afya sana kwao
Dk 86 Yanga wanapata kona ya kwanza katika kipindi cha pili, inachongwa na MSuva lakini inaokolewa na kuwa ya mpira wa kurushwa
SUB DK 85, Ayubu Yanga ambaye ni Mtanzania anaingia zikiwa zimebaki dakika 5 katika kipindi hiki cha pili
SUB Dk 83, Justine Zulu anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Deus Kaseke
Dk 81 sasa, kidogo Yanga wanaonekana kutulia na kuanza kugongeana vizuri


GOOOOOO Dk 78, Zanaco wanapata bao la pili kwa shuti kali mfungaji akiwa ni KWame raia wa Ghana ambaye aliunganisha krosi safi kabisa baada ya Zanaco kushambulia kwa dakika nzima mfululizo
Dk 76, Yanga wanatakiwa kuwa makini maana wanaruhusu krosi nyingi langoni mwao na Zanaco wanaonekana kushambulia mfululizo
Dk 75 Yanga wanafanya shambulizi tena, Msuva anajaribu kuuwahi mpira, shuti lake linagonga nyavu za pembeni kwa nje

Dk 75, pasi nzuri ya Msuva, Martin anaachia mkwaju safi kabisa, unatoka pembeni kidogo
Dk 73, shambulizi jingine la Zanaco, Musonda tena lakini anapiga shuti dhaifu, Dida anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 73, Musonda anaachia mkwaju unaokolewa, anaachia mwingine unaokolewa
SUB Dk 69 Kennedy Musonda anaingia kuchukua nafasi ya Sakala


Dk 69 Zanaco wanapata kona na wanaonekana kama Yanga wamechanganyikiwa, maana wanapoteza pasi hovyo na hali ya kujiamini hasa katika kiungo tokea atoke Kamusoko inaonekana kuporomoka
Dk 68, Kwame anamnyanyasa Bossou, anamtambuka ndani ya boksi lakini mkwaju wake ni dhaifu
Dk 67, Mulenga anaingia vizuri na kuachia mkwaju mkali sana. Bahati nzuri kwa Yanga ni kwa kuwa haukulenga lango tu


Dk 65 Faulo matata inachongwa hapa, Dida anaruka na kuukosa. Unatoka nje kidogo tu, ilikuwa hatari sana
Dk 64 Zanaco wanaingia, Sakala anamtoka Kessy lakini Bossou anawahi na kuokoa lakini anashika. ni faulo karibu na lango la Yanga, si sehemu nzuri kwa Yanga
Dk 63, Martin anapata nafasi kutokana na kuwazidi kasi mabeki wa Zanaco lakini anapiga shutu dhaifu na kuwa goal kick
SUB Dk 60, Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Thabani Kamusoko
SUB Dk 58, Ngoma anakwenda kwenye benchi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
DK 57 sasa, mpira umesimama baada ya beki wa Zanaco kugongana na Ngoma wakati wakiwania mpira
KADI Dk 53, Kessy anamkwatua Sakala na mwamuzi anamlamba kadi ya njano


Dk 51, Mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na inaonekana Zanaco ndiyo wanaotaka zaidi bao kutokana  na kasi yao
Dk 49 Chirwa anaachia mkwaju unakwenda juuu. Ndiyo shambulizi la kwanza la Yanga kipindi hiki
Dk 48, Kwame wa Zanaco anawachambua mabeki wa Yanga na kuachia mkwaju lakini ni dhaifu
Dk 46, Zanaco wanafanya shambulizi kali tena, faulo. Wanapata mkwaju wa faulo lakini Mbwebya anapaisha juuuu kama ile ya kipindi cha kwanza
 
DK 45, Zanaco wanaanza kwa kasi kubwa, Sakala anamtoka Bossou na kupiga krosi lakini Dida anakuwa makini







MAPUMZIKO
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 45, shambulizi jingine la Yanga lakini Zanaco wanaokoa na wanaonekana kuingia uoga
KADI Dk 43, mwamuzi anamwita Sakala na kumlamba kadi ya njano, inaonekana aliingia uwanjani bila ya ruhusa wakati alipotoka kutibiwa
Dk 42, Sakala wa Zanaco alikuwa chini amepatwa na maumivu, ameishapata matibabu na sasa mechi inaendelea. Inaonekana waamuzi wameitana na kuanza kujadiliana
GOOOOOOOOOO Dk 39, Ngoma anampa Zulu, anayetoa pasi maridadi kwa Msuva ambaye anaingia na kuachia mkwaju mzuri wa ufundi unaomshinda kipa wa Zanaco na kujaa wavuni
KONA Dk 37, Mwinyi analazimika kulala na kuokoa, kona ya kwanza ya mchezo

Dk 36, Mulenga anaingia kwa kujiamini katika lango la Yanga na kuachia mkwaju mkali. unapaa, ilikuwa ni hatari



Dk 36, Yanga wametulia na kuanza kupanga mashambulizi lakini wanaonekana kukosa utulivu wanapokuwa kwenye eneo la hatari la Zanaco. Lazima watulie
Dk 35, Yanga wanaendelea kuonyesha wameamka, wanagongenaa vizuri lakini pasi ya mwisho ya MSuva ndani ya eneo la hatari inakosa mtu baada ya Chirwa kuwa amesimama
Dk 33, Kamusoko anawafinya mabeki wawili wa  Zanaco na kumuachia Ngoma lakini anaachia shuti kuuuubwaaaaa nje
Dk 31 mpira mrefu wa Kessy lakini kichwa cha Msuva kinaenda nje
Dk 31 Yanga wanaingia vizuri, mpira wa adhabu wa Kessy, kipa wa Zanaco anaokoa kichwani mwa Cannavaro
Dk 28, Zanaco wanapelekwa shambulizi jingine, ilikuwa hatari kwenye lango la Yanga huku mabeki wakionekana kutotulia. 

Dk 26 Kamusoko anageuka kwa kujiamini, anaachia mkwaju mkali kabisa na kuwa goal kick. Hili ndiyo shambulizi kali zaidi la Yanga hadi sasa





Dk 25 sasa, Yanga wanaonekana kutijiamini, hawachezi kama wako nyumbani wakipoteza mpira kila baada ya pasi tatu au nne na Zanzo wanaonekana kuwa wametulia utafikiri ni wenyeji wakisukuma mashambulizi mengi zaidi
Dk 22 Sakala anaruka na kupiga kichwa, mpira unapanguliwa na Dida na kugonga mwamba na mwamuzi anasema tayari ilikuwa ni offside


Dk 22, Kasonde anaachia mkwaju mkali kabisa lakini unawababatiza mabeki wa Yanga na kudaka
Dk 19, mkwaju mkali wa Mbewembya unapita juu, huyu ndiye alifunga bao Zanaco ikiitoa APR. Ilikuwa ni bao la mkwaju wa adhabu kama huu
Dk 17, Mulenga anaingia na kuachia mkwaju lakini unakuwa ni dhaifu

Dk 12 Dida anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la karibu kutoka kwa Sakala ambaye aliingia vizuri akiichambua difensi ya Yanga




Dk 11, Yanga wanapata nafasi nzuri lakini Kamusoko anashindwa kuitumia
Dk 10, Justine Zulu anageuka na kuachia mkwaju mkali kabisa kwenye lango la Zanaco lakini ni goal kick
Dk 7, Ernest Mbewe anawatoka mabeki wa Yanga, lakini Mwinyi anaokoa. Huyu jamaa ni hatari na ana kasi sana
Dk 6, krosi safi ya mpira wa adhabu Kessy, Ngoma na Msuva wanajichanganya wenyewe

Dk 5, Tembo ambaye ni beki anaingia kwa kasi lakini Yanga wanaonekana kushituka, kasi inaonekana kuwa kali kila upane
Dk 2, Zanaco wanaanza kuonyesha cheche baada ya Chirwa wa Zanaco kuingia vizuri lakini Mwinyi akambana vizuri

Dakika ya 1 tu, Zanaco wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Yanga, mpira unatolewa na kuwa wa kurushwa

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment