Majibu Ya Mwakyembe Kuhusu Ripoti Ya Kamati Ya Nape

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe leo amezungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma mara baada ya kukaribishwa rasmi Wizarani hapo..

Baada ya maongezi aliruhusu mwaswali ambapo moja ya swali aliloulizwa na wanahabari ni kuhusu ripoti iliyoachwa na Waziri wa zamani Nape Nnauye kuhusu uchunguzi wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kudaiwa kuvamia ofisi za Clouds Media huku akiwa na Askari wenye silaha.

==>Haya ni majibu aliyoyatoa
"Wengi mnauliza nimeifanyia kazi gani ripoti ya Nape, mimi hiyo ripoti sijaiona na kama mwanasheria kwangu ni mwiko na sitapeleka taarifa ambayo haijakamilika.

"Kupitia vyombo vya habari taarifa imeeleza kuwa ushahidi ulitolewa na upande wa Clouds Media na mkakiri kuwa upande wa pili haukupatikana.
"Huwezi kuwa Hakimu kwenye suala lako wewe mwenyewe, kufanya hivyo ni ubatili kwahiyo hata mimi ningekuwa ni mwandishi wa habari ningesema hili jambo siliwezi kwakuwa linanihusu na mimi.

"Kanuni zinataka kusikiliza upande wa pili, sasa mmeshasema kitu kina upande mmoja alafu nimpelekee kiongozi wangu..NO, mimi kazi yangu ni kupata maelezo ya upande wa pili na nitapata.

"Hili jambo ni lakufa na kupona, yani niache kukutana na wakuu wa idara mbalimbali hapa kuhakikisha nakuza suala la sanaa na kuhakikisha vijana wetu hawaendelei kuibiwa nibaki kuhangaikia suala la ripoti.

"Mimi sikuapa kwa jambo hilo moja pekee lakini mimi ni mwanasheria mkongwe na nitahakikisha nalifuatilia lakini mimi sitaunda kamati katika jambo hilo.

"Lengo letu ni kuhakikisha hatutakuwa na matukio ya namna hiyo katika safari lakini tukitoka na kauli za papara tutakuwa tunajitafutia matatizo hapo mbeleni "
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment