Jana kumetokea mauaji ya kikatili ya mwanafunzi anayesoma chuo kikuu cha IFM. Mwanafunzi huo kwa mujibu wa habari tulizozipata anajulikana kwa jina la Khamis Twaha Hechi. Usiku wa Jumapili Twaha akiwa chumbani kwake alivamiwa na watu wanaodaiwa kuwa ni vibaka. Aliporwa simu yake na wakati akijaribu kujihami wakamchoma kitu chenye ncha kali shingoni.
Wakati jitihada za kumpeleka hosptali zikifanyika alikuwa akivuja damu nyingi hali ambayo imepeplekea kupoteza maisha. Baadhi ya picha ambazo nimezipata kupitia mitandao ya kijamii ni hizi hapa.
0 comments :
Post a Comment