Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dr Jakaya Kikwete anazindua taasisi yake muda huu. Miongoni mwa timu ya taasisi hiyo ni Prof Mahalu ambae ni daktari bingwa wa moyo, Mkandara na Ombeni Sefue huku Kikwete akiwa mwenyekiti wa taasisi. Bodi ya taasisi hiyo pia imejumuisha wajumbe wengi kutoka nje ya nchi.
Hii inakuwa taasisi ya tatu inayoanzishwa na kubebwa na majina ya marais wastaafu ikitanguliwa na taasisi za Mwl Nyerere(Mwl Nyerere Foundation) na Mkapa Foundation huku Mwinyi yeye akipita kimya kimya.
Kulingana na taasisi hiyo, itajihusisha na afya hasa ya mama na mtoto, kudhibiti Maleria na lishe bora. Pamoja na hayo taasisi hiyo itajihusisha na elimu hasa ya vijana, kukuza vipaji, ujasiriamali na mafunzo. Mratibu wa taasisi hiyo, Omary Issa ambaye aliteuliwa na JK wakati wa utawala wake kuongoza 'Matokeo makubwa sasa' amesema Kikwete ameamu kutoa utaalamu na maarifa yake kwa watanzania na waafrika kwa ujumla.
Wengine katika taasisi hiyo ni Jack Steve ambae ameshawahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania, Aboubakar Bakhresa ambae ni mfanyabiashara, Indriss Jala ambae ni waziri katika serikali ya Malaysia, Kisangugi ambae ni mmarekani mwenye asili ya Tanzania na mfanyibiashara.Rais
0 comments :
Post a Comment