Nimeona interview ya Clouds TV na Mzee Platnumz, kweli jamaa kachoka. Huyu ni Baba yake na mwanamuziki matata nchini Diamond Platnumz.
Kama alikukosea wewe na mama yako, mbona ameshasema mumsamehe? Bila ya yeye Diamond asingekuwa alivyo sasa. Hivyo inatakiwa Diamond awe na moyo mkubwa wa kusamehe mtu ambaye ameshaomba kusamehewa. Binadamu tuna mapungufu na ni ujasiri ulioje kukubali kuwa umekosa na kuomba kusamehewa.
Diamond ni kioo cha jamii, uwe na moyo wa kusamehe. Pia kwa Queen Darlin, Baba yenu kawaomba msamaha wote.
Msaidieni Baba Yenu ana Hali Mbaya
0 comments :
Post a Comment