Rais Wa Sudani Kusini Atubu


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, ameongoza maelfu ya raia nchini humo kwa ajili ya maombi maalum ya toba.

Ni sauti ya Rais Kiir, katika maombi maalum ya toba yaliyofanyika kwenye makumbusho ya kiongozi wa zamani wa taifa hilo John Garang, mjini Juba ambapo kwa niaba ya serikali Rais huyo ameomba toba kwa taifa lake na kumsihi Mungu awaepushie hukumu na kuwasamehe.

''Mungu wa mbinguni naomba msamaha kwa lolote nililofanya katika mamlaka yangu.'' Amesema Rais Kiir katika sehemu ya maombi yake kwa Sudan Kusini, taifa ambalo limeghubikwa na migogoro kwa takribani miaka minne sasa.

Aidha Rais Kiir katika maombi hayo, alikabidhi moyo na mwili wake kwa ajili ya baraka na kuomba msamaha kwa niaba ya uongozi wa juu wa taifa hilo.

''Tafadhali Mungu nakuomba nifanye chombo cha upendo ,utekelezaji , upatanishi na msahama'' Rais huyo amesikika akiomba.

Katika hatua nyingine wakati wa maombi hayo, Rais Kiir amewasamehe na kuamuru kuachiliwa kwa Gavana wa jimbo la Wau Elia Waya na kaimu wake Andrea Dominic ambao wamekuwa kizuizini tangu Juni 2016.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment