Wachezaji Wanne Wa Yanga Kuikosa Mtibwa Kesho


WASHAMBULIAJI wa timu ya Yanga Donald Ngoma, Amiss Tambwe na Matheo Anthony hawatakuwepo kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na kuwa majeruhi huku Obrey Chirwa akibakia jijini Dar kutokana na adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.
Yanga itashuka dimbani kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro katika mchezo wa ligi ambapo huku ikiwa nyuma kwa pointi mbili dhidi ya vinara Simba ambao jioni ya leo watacheza na Mbeya City kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kukosekana kwa washambuliaji hao kutamfanya kocha George Lwandamina kubadili mfumo wa uchezaji ambapo anaweza kumtumia Emmanuel Martin na mmoja kati ya Haruna Niyonzima au Juma Mahadhi kama washambuliaji wa kati huku Deus Kaseke Deus Kaseke na Simon Msuva wakishambulia kutokea pembeni.
Meneja wa timu hiyo Hafidh Saleh ameiambiaBOIPLUS kuwa kikosi hicho kitasafiri leo kuelekea mkoani humo bila ya nyota hao lakini wakijiamini kuibuka na ushindi kwa kuwategemea nyota wengine waliopo kikosini humo.
“Kikosi cha Yanga kitasafiri leo kuelekea Moro kwa mchezo wetu na Mtibwa lakini tutawakosa Ngoma, Tambwe na Matheo ambao ni majeruhi, ila tuna kikosi kipana tutawatumia nyota wengine na tuna uhakika wa kuibuka na pointi tatu” alisema Hafidh.
Msuva anategemewa kuwa uti wa mgongo wa mashambulizi ya timu hiyo akitokea pembeni kutokana na kasi aliyonayo ambapo kama Mtibwa wataweza kumdhibiti nyota huyo basi mchezo unaweza kuwa mgumu kwa upande wa Yanga.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment