Baadhi
ya wasanii wa kundi la Mama Ongea na Mwanao, waliokuwa katika kampeni
za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 za mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mama Samia Suluhu, wamekanusha madai ya kutolipwa wala kukidai
chama hicho madeni yoyote wakati na baada ya kampeni hizo kumalizika.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam leo, Makamu Mwenyekiti
wa muda wa kundi hilo, Yobnesh Yusuph maarufu Batuli, alisema madai hayo si kweli kwani wasanii wote walilipwa na mikataba wanayo.
“Nikiwa
kama Makamu Mwenyekiti wa ‘group’ hili la Mama Ongea na Mwanao kwa
muda, ni kweli kuna uvumi ulienea katika mitandao kwamba wasanii
tulioshiriki kampeni na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu hatujalipwa,
si kweli nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli.
“Ingawa
kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani, wapo wanaoshawishiwa
kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais na kuichafua CCM, mimi
nakataa, wasanii wote tulilipwa na mikataba ipo.
"Haiwezekani wewe staa mkubwa unakaa mbele ya vyombo vya habari unaongea uongo kwamba wasanii hatujalipwa wakati wewe ndiyo ulikuwa unawalipa hicho kitu hakiwezekani,” alisema Batuli aliyekuwa ameongozana na baadhi ya wasanii wa kundi hilo.

0 comments :
Post a Comment