Hatima
ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema),
itajulikana Ijumaa wiki hii baada ya shauri hilo kurudishwa Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha kwa utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa.
Hatua
hiyo imekuja baafa ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa
Tanzania kufuta rufaa mbili za Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), dhidi ya
mbunge huyo juzi mjini hapa.
Mmoja
wa mawakili anaomtetea mbunge huyo, Adam Jabir, alisema shauri hilo
litaamuliwa Machi 3, mwaka huu mbele ya Jaji Salma Maghimbi kutokana na
rufaa ya Jamhuri namba 135 ya mwaka jana, inayopinga uamuzi wa Novemba
11, mwaka jana wa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi
Kamugisha kumpa Lema haki ya dhamana.
Novemba
11 mwaka jana, Wakili Mwandamizi wa Serikali Paul Kadushi, alisimama
wakati hakimu huyo akijiandaa kuandika masharti ya dhamana na kuieleza
mahakama hiyo kuwa wameshasajili notisi ya kusudio la kukata rufaa
Mahakama Kuu wakipinga uamuzi wa hakimu huyo kumpa Lema dhamana.
Hata hivyo,uamuzi huo wa dhamana haukuweza kutekelezwa kwa sababu ya nia ya kukata rufaa waliyoitoa mawakili hao wa Serikali.
Hakimu
Kamugisha alishindwa kuendelea na mahsarti ya dhamana kwa mshitakiwa
huyo ambapo,alikubaliana na upande wa Jamhuri na kusema kuwa notisi ina
hadhi sawa na maombi ya rufaa yaliyowasilishwa Mahakama Kuu hivyo
mwenendo na uamuzi wake utasimama mpaka uamuzi utakapotolewa na Mahakama
Kuu.
Januari
4 mwaka huu, Jaji Maghimbi alitarajiwa kusikiliza na kutoa uamuzi
kuhusiana na dhamana ya Lema ila ilikwama baada ya mawakili wa Serikali
kukata Rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania,kupinga Jaji huyo kusikiliza
rufaa yao wenyewe.
Jaji
Magimbi alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa iliyowasilishwa na upande
wa Jamhuri wakipinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumpa Lema haki ya
dhamana.
Uamuzi
huo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wakazi wengi wa jiji la Arusha,hasa
ikizingatiwa mbunge huyo anashikiliwa katika mahabusu ya Gereza Kuu la
Kisongo kwa zaidi ya miezi mitatu,tangu akamatwe na polisi nje ya
viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Novemba 2, mwaka jana.
Aidha
uamuzi huo ulikuwa unatarajiwa kutoa tafsiri ya kisheria ya notisi ya
nia ya kukata rufaa iliyowasilishwa na na mawakili hao wa Jamhuri,notisi
iliyosababisha Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi kutokuendelea na hatua ya
kuweka masharti ya dhamana.
Akiahirisha
uamuzi huo mahakamani hapo,Jaji huyo alisema kuwa mikono yake imefungwa
na hawezi kusikiliza na kutoa uamuzi kutokana na mawakili wa
Serikali,kusajili nia ya kusudio la kukata rufaa Desemba 30 mwaka
jana,katika Masijala ya Mahakama ya Rufaa Tanzania iliyopo mkoani hapa,
kupinga asisikilize rufaa hiyo.
Awali
kabla ya mawakili wa serikali kukata rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania
kupinga kusikilizwa kwa rufaa yao Mahakama Kuu, Jaji Maghimbi,aliwataka
mawakili wa Jamhuri kuwasilisha hoja zao za rufaa Disemba 29,huku
mawakili wa Lema wakitakiwa kujibu hoja hizo Disemba 30 kabla ya
mahakama hiyo kutoa uamuzi wa rufaa hiyo jana.
Lema
anakabiliwa na kesi mbili za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli,
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kesi namba 440 na 441.
0 comments :
Post a Comment