Simba Na Azam Fc Kutunishiana Misuli Kesho




KESHO Jumamosi, Simba inaingia uwanjani kupambana na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA, tayari Wekundu hao wa Msimbazi wamewashika pabaya wapinzani wao, huku wakipania kuvunja mwiko wa kutoshiriki michuano ya kimataifa kwa takriban miaka minne.

Timu hizo zitapambana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, ambapo kuelekea mchezo huo Simba imeweka kambi mkoani Morogoro huku Azam ikijichimbia kwenye uwanja wao wa Azam Complex jijini Dar.

Simba ambayo kwa takriban miaka minne haijashiriki michuano ya kimataifa, kesho itaingia uwanjani kuhakikisha

inashinda ili iweze kucheza fainali na hatimaye kuchukua kombe hilo waweze kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, msimu ujao.

Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ameweka bayana mikakati yao kuelekea mchezo huo huku
akisema tayari wametambua mbinu za wapinzani wao watakazoingia nazo uwanjani siku hiyo.

“Unajua tegemeo pekee la Azam ili msimu ujao wacheze michuano ya kimataifa limebaki katika Kombe la FA, hivyo ni lazima wataingia kwa nguvu zao zote wakisaka ushindi ili tu waweze kuibuka washindi na kuingia fainali.

“Kutokana na hali hiyo, sisi pia tumejipanga kwa hali hiyo na kwa kuwa tumeshajua mbinu zao, itakuwa rahisi kwetu kupambana nao na kuwashinda,” alisema Mayanja.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment