Simba Yawasilisha Rufaa Yake Mechi Ya Kagera

17757413_399065340474753_2338452281136611112_n
Unaweza kusema mambo yamekucha baada ya uongozi wa klabu ya Simba, kuwasilisha rufaa Bodi ya Ligi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukidai pointi za mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Jumamosi.

Katika mechi hiyo, Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1, lakini Simba inadai Kagera Sugar walimchezesha beki  Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano.
Kamati ya masaa 72 inatarajiwa kukutana kesho na imeelezwa tayari Simba ilishawasilisha rufaa hiyo.
Hata hivyo, Kagera Sugar imesisitiza kuwa Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano.
Awali, Kocha Mecky Maxime alisisitiza gilo lakini Mohammed Hussien naye akasisitiza wana uhakika Fakhi ana kadi mbili za njano.
Katika mechi hiyo, Fakhi aliyewahi kuichezea Simba, alikuwa mmoja wa mabeki vizingiti dhidi ya washambuliaji wa Simba.
Ilikuwa ni mechi ya ushindani na Kagera walionyesha soka safi na kuishinda Simba.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment