Yanga Yasikitisha Wadau Wa soka Dodoma

UONGOZI wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Dodoma (DOREFA) umesikitishwa na kitendo cha klabu ya Yanga kupeleka timu ya vijana badala ya wakubwa kama walivyokubaliana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini ya Polisi Dodoma uliofanyika leo.

Mwenyekiti wa DOREFA Mulamu Ng’ambi amsema kuwa kitendo walikichofanya Yanga si cha kiungwana na hakikupaswa kufanywa na klabu kubwa kama hiyo kwani mashabiki wengi walijitokeza kuwashuhudia nyota wa mabingwa hao watetezi wa ligi ya Vodacom lakini imekuwa tofauti hali ambayo ingeweza kupelekea uvunjifu wa amani.

“Kiukweli Yanga wametuangusha sana leo, tulipatana walete timu ya wakubwa na tayari tulishawalipa pesa ya awali lakini imekuwa tofauti na hawakutupa taarifa yoyote. Bora hata wangeleta kikosi cha akiba lakini wametuletea timu ya vijana kweli? wametusikitisha sana.

“Mashabiki walijitokeza wengi sana lakini wengine kabla ya kuingia wakasikia timu iliyokuja ni ya vijana hawakuingia, na walioingia walikuwa wakipiga kelele wanadai pesa zao sasa suala hili linaweza kuvuruga amani hasa kunapokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu,” alisema Ng’ambi.
Akijibu tuhuma hizo Katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa alisema wameshindwa kupeleka kikosi cha kwanza kutokana na ratiba ya kombe la FA ambapo wanatakiwa kusafiri kwenda jijini Mwanza kucheza na Mbao FC Jumapili katika mchezo wa nusu fainali.

“Tulikubaliana na DOREFA kabla ya ratiba ya FA haijatoka juzi Jumapili kwa hiyo hatukuwa na jinsi lakini tutakuwa na vikao kwa ajili ya kujadili jambo hili kabla ya kulitolea ufafanuzi baadae,” alisema Mkwasa.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani humo timu hizo zilitoka sare ya bao moja.

Kwa upande wake waziri wa habari, sanaa,utamaduni na michezo Mh Mwakyembe amesema  hajafurahia kitendo cha yanga kupelekeka timu ya vijana badala ya wakubwa hivyo amewataka viongozi wa yanga kutoa maelezo kwa nini imekuwa hivyo.

waziri mwakyembe ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo aliondoka uwanjani akionesha amekasirika kabla ya mchezo huo kumalizika.

Mchezo huo ulimalizika kwa matokoea ya yanga 1-1 Majeshi mchanganyiko.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment